KITENGO CHA MANUNUZI
MAJUKUMU YA KITENGO CHA MANUNUZI
1. Kutoa ushauri/mapendekezo kuhusu masuala yote yanayohusu manunuzi kulingana na sheria ya ununuzi wa umma No.7 ya 2011 na kanuni zake za Desemba 2013 GN NO 446.
2. Kuandaa mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia uhitaji na matakwa ya kila Idara ka kuzingatia bajeti.
3. Kupokea mahitaji ya ununuzi wa bidhaa na huduma tokea Idara tumiaji ( User department) na kutekeleza ununuzi wake kulingana na taratibu na kanuni za manunuzi ya Umma.
4. Kufanya zoezi la kuhesabu mali wakati wa kufunga hesabu za mwisho wa Mwaka.
5. Kuandaa mikataba mbalimbali kwa kazi za wakandarasi/ bidhaa na huduma kwa Idara mbalimbali.
6. Kupokea vifaa, bidhaa mbalimbali tokea kwa watoa huduma na kuzigawa kwa wahitaji kulingana na mahitaji yao.
7. Kutunza kumbukumbu mbalimbali zinazohusiana na manunuzi ya bidhaa au huduma.
8. Kuwianisha ubora wa bidhaa na thamani ya fedha .
9. Kutekeleza kazi zote za zabuni kwa kuzingatia uwazi,usawa na uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote wanohusika na manunuzi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.