• Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Handeni Town Council
Handeni Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • kilimo
    • ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • fedha na uongozi
      • mipango miji na mazingira
      • uchumi afya na elimu
      • ukimwi
      • maadili
    • Ratiba
      • vikao vya waheshimiwa madiwani
      • kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo Mbalimbali
    • fomu mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio

Zoezi la ugawaji vishikwambi kwa walimu lakamilika Halmashauri ya Mji Handeni

Posted on: January 13th, 2023

Leo tarehe 13 Januari 2023 ikiwa ndiyo siku ya mwisho ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu ugawaji wa vishikwambi kwa walimu, waratibu Elimu kata na maafisa Elimu ngazi ya Halmashauri, Halmashauri ya Mji Handeni ilipokea jumla ya vishikwambi 319 vilivyotumika katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na  imegawa vishikwambi  vyote 319 kwa mchanganuo ufuatao  vishikwambi vitatu(3) wamepatiwa maafisa elimu ngazi ya Halmashauri, vishikwambi kumi na mbili(12) wamepatiwa waratibu Elimu kata na vishikwambi 304 wamepatiwa walimu wa shule za msingi na sekondari. Hata hivyo jumla ya idadi ya walimu wote katika Halmashauri ya Mji Handeni ni 588 ikiwa waliopata vishikwambi ni 304 sawa na asilimia 51.7 na upungufu ukiwa ni vishikwambi 284 sawa na asilimia 48.3 ya walimu wote ambao hawajapata vishikwambi.

Akizungumza wakati wa  kupokea vishikwambi hivyo Mwalimu Goefrey William Daiford kutoka shule ya Sekondari Kileleni  amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha sekta ya Elimu Nchini ambapo kutokana na vishikwambi changamoto mbalimbali zinakwenda kutatuliwa ikiwemo kupata dhana tofauti kutoka mtandaoni na kuweza kutunza kumbukumbu katika vishikwambi na hivyo kuongeza ufanisi kwenye kutoa Elimu wakati huohuo amewaahidi wazazi na walezi wategemee wanafunzi kupata Elimu iliyo bora na ya kisasa kwani kuwepo kwa vishikwambi kutaongeza ubora wa Elimu inayotolewa.

Mwalimu Goefrey William Daiford(kulia) akipokea vishikwambi kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari vifaa na takwimu Bw Montan Mathew(kushoto).

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi. Maryam Ukwaju amewasisitiza walimu kuzingatia utaratibu uliowekwa juu ya matumizi sahihi ya vishikwambi kama ifuatavyo:-

  1. Vishikwambi hivi ni maliya serikali, hivyo vitasimamiwa kwa mujibu wa sharia ya Manunuzi ya Umma na kanuni zake zinazohusu matumizi ya Mali za Umma.Endapo Mwalimu au kiongozi wa Elimu atakoma kuwa Mtumishi wa Umma kwenye kada ya ualimu(kustaafu, kufukuzwa, kuacha kazi au kufariki), au kuhama kada ya ualimu,atalazimika kukabidhi kishikwambi hicho kwa Mkuu wa kituo chake cha kazi;
  2. Vishikwambi hivi ni kwa ajili ya matumizi ya kujifunzia na kufundishia kwa walimu wa shule za msingi na sekondari hivyo, matumizi mengine, kama vile kuwapiga picha wanafunzi na kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii, kupiga picha kwenye harusi na sherehe mbalimbali zisizohusu ujifunzaji na ufundishaji hayaruhusiwi;
  3. Vishikwambi hivi vigawiwe kwa walimu wote walio kwenye ajira ya kudumu ya serikali; na
  4. Mwalimu anaruhusiwa kutumia picha za video na matini za masomo(lesson notes) alizozichuja au kuchukua kutoka Taasisi ya  Elimu Tanzania katika kufundishia ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.

Na mwandishi wetu

Handeni Mji

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI UJENZI WA JENGO LA DHARURA (EMD) HOSPITALI YA WILAYA HANDENI February 16, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • Afisa elimu msingi: Kula shuleni ni lazima

    March 13, 2023
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yafana, Halmashauri ya Mji Handeni

    March 08, 2023
  • Walimu Halmashauri ya Mji Handeni, wapata mafunzo ya mfumo wa FFARS

    March 04, 2023
  • MILIONI 63.6 ZAMWAGWA KWA WAJASIRIAMALI HANDENI MJI. RAIS SAMIA ATAJWA.

    March 03, 2023
  • Angalia zaidi

Video

Mbunge wa jimbo la Handeni Mjini Mh.Reuben Kwagilwa aliamsha Bungeni
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Kumuona Mkurugenzi
  • Kupata kibali cha Matangazo
  • Muundo wa Tasisi
  • Kumuona Mwenyekiti wa Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Sekretariti ya Ajira
  • Ofisi ya Rais - Ikulu
  • FFARS-LIVE
  • PLANREP- BAJETI 2020/21
  • TAMISEMI
  • Utumishi

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani

Wasiliana na sisi

    Barabara ya Korogwe - Handeni

    Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI

    Simu ya Mezani: 027-2641807

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: td@handenitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.