Akifungua wiki ya Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni, na kuhudhuriwa na wakuu wa idara pamoja na watendaji wa kata na mitaa wote wa Halmashauri ya Mji Handeni, inayoanza leo tarehe 11 Julai 2023 Mkuu wa Wilaya Handeni, Wakili Albert Msando amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi.Maryam Ukwaju kwa kukusanya Mapato kwa asilimia 104 kwa mwaka wa fedha 2022/23. Hii imetokana na ushirikiano mkubwa uliokuwepo baina yake, watumishi na watendaji wote wa Halamashauri ya Mji.
Aidha amewakumbusha kuwa kuna vyanzo vingine bado havijafanyiwa kazi, kama vile bodaboda, mafundi seremala na wauza mkaa hawa wakisajiliwa wataipatia Halmashauri mapato. Pia aliawaambia kuwa kuanzia Januari 2024 kodi za majengo zitakusanywa na Halmashauri na kumtaka Mkurugenzi kuanza maandalizi pamoja na kuwaelimisha wananchi kuhusu kodi hiyo
Mheshimiwa mkuu wa wilaya ametoa rai kuwa, watendaji kupewa mafunzo ya kutumia Mfumo wa TAUSI na namna ya kutoa leseni ili watoe leseni za biashara kwa wananchi bila kuja Halmashauri kwa kuwa vitu vyote sasa vinapatikana kwenye mtandao, hili linaweza kufanyika kwa awamu ili kujua na kuona changamoto mbalimbali wakati wa kulitekeleza.
Wajumbe wa kamati za ukusanyaji mapato waliohudhuria katika uzinduzi wa wiki ya Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni
Nae Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Husseni Omari Khatibu(Diwani) alisema, kukusanya mapato ni mojawapo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo tufanye kazi kwa ushirikiano na kukusanya mapato tutaweza kukamilisha miradi na kuwaletea wananchi maendeleo.
Mwisho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi.Maryam Ukwaju aliwaasa kuwa, wasiridhike kwa kukusanya mapato asilimia 104, bali waongeze juhudi na kubuni vyazo vingine vya mapato ili kufikia lengo, aidha aliwakumbusha kujiandaa kukusanya kodi ya majengo kuanzia Januari 2024 kama ambavyo Serikali imeirudisha makusanyo hayo kwenye Halmashauri kwa ajili ya ukusanyaji.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.