Shirika la Islamic Help linalojihusisha na utoaji misaada, yenye makao yake makuu nchini Uingereza, limetoa msaada wa ng'ombe zaidi ya 350 kwa wanachi katika Halmashauri ya mji Handeni na ng'ombe 1600 kwa mkoa wa Tanga kiujumla, kwa ajili kitoweo katika kusheherekea sikukuu ya Eid Al Adha.
Akizungumza wakati wa kuwashukuru wahisani hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni, Mh.Mussa Abeid Mkombati(Diwani) amesema, uhusiano mzuri wa kimataifa uliojengwa na unaoendelea kujengwa na Rais wa awamu ya sita Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan kati ya nchi yetu na nchi nyingine ndio uliowashawishi wahisani kuiona Handeni na kuja kuleta msaada huo.
Mratibu msaidizi wa zoezi la ugawaji nyama kutoka Islamic Help, Habibu Mbota kulia,akizungumza mbele ya Mwenyekiti waHalmashauri ya Mji Handeni Mh.Mussa Mkombati(Diwani)
Nae Katibu Mtendaji wa shirika hilo, Mustafa Emim Saglam amesema mbali na kutoa msaada wa kitoweo hicho katika kipindi hiki cha sikukuu, pia wamekuwa wakitoa msaada wa kuchimbia visima vya maji katika maeneo mbalimbali wilayani Handeni, kazi ambayo wanaendelea nayo.
Kwa upande mwingine, Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Handeni Athumani Kitabala amewahakikishia wananchi kuwa kila Ng'ombe hupimwa afya yake kabla ya kuchinjwa na nyama hukaguliwa baada ya Ng'ombe kuchinjwa, hivyo kitoweo wanachogaiwa ni salama kwa afya ya mlaji.
Wananchi wa Kata ya Kwamagome wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni, Mh.Mussa Mkombati(Diwani), hayupo pichani,wakati wa zoezi la ugawaji nyama.
Wakati huohuo wananchi wa maeneo mbalimbali mjini Handeni, wameishukuru Taasisi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wao katika Halmashauri ya Handeni Mji kwa kufanikisha msaada huo kuwafikia katika kipindi hiki cha sikukuu.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.