• Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Handeni Town Council
Handeni Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • kilimo
    • ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • fedha na uongozi
      • mipango miji na mazingira
      • uchumi afya na elimu
      • ukimwi
      • maadili
    • Ratiba
      • vikao vya waheshimiwa madiwani
      • kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo Mbalimbali
    • fomu mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio

Marry Mntambo Chambuya(CCM) Mshindi uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Vibaoni , Halmashauri ya Mji Handeni

Posted on: December 17th, 2022

Uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata ya vibaoni uliofanyika leo tarehe 17-12-2022 umetamatika kwa wananchi wa kata ya vibaoni yenye mitaa mitano(5) na vituo 12 vya kupigia kura, kumchagua Ndugu. Marry Mntambo Chambuya(CCM) kuwa diwani mteule wa kata ya vibaoni kwa kura 1400 dhidi ya mshindani wake Ndugu Hilaly Seif Kitwanga wa chama cha wananchi CUF aliyepata kura 214.


Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi mdogo wa kata ya vibaoni kwenye ofisi za kata ya vibaoni, msimamizi msaidizi wa uchaguzi Bi. Zainabu Mhanga amesema jumla waliojiandikisha kupiga kura ni 4186, waliopiga kura ni 1654 , kura halali ni 1614 na kura zilizoharibika ni 40.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya vibaoni Bi. Zainabu Mhanga akitangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata ya vibaoni mbele ya wananchi waliojitokeza kusikiliza matokeo hayo kwenye ofisi za kata ya vibaoni.


Akizungumza mara baada ya kutangazwa matokeo hayo, mshindi wa uchaguzi huo mdogo wa udiwani Bi. Marry Chambuya amewashukuru wapiga kura wote waliojitokeza siku ya leo, wasimamizi wa uchaguzi, na viongozi mbalimbali walioshiriki katika zoezi zima la uchaguzi. Ameahidi kuwa kiongozi wa wananchi wote wa kata ya vibaoni bila ubaguzi wa aina yoyote.


Nae msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Handeni mjini ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya mji Handeni Bi.Maryam Ukwaju, amewashukuru wananchi wa kata ya vibaoni kwa kujitokeza na kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kumchagua diwani wa kata yao katika hali ya utulivu na amani. Pia amewashukuru viongozi wa ulinzi na usalama kwa kazi nzuri ya kulinda amani kipindi chote cha kampeni, siku ya kupiga kura mpaka wakati wa kutangazwa kwa matokeo.

Msimamizi mkuu wa Uchaguzi wa Jimbo la Handeni Mjini ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Handeni Bi. Maryam Ukwaju akizungumza na wananchi waliojitokeza mara baada ya matokeo kutangazwa.


Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mji Mh. Mussa Mkombati(Diwani CCM) amesema ameupokea ushindi wa Bi.Marry Chambuya kwa furaha kubwa huku akisema kuwa hayo yametokana na matunda ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais wake Daktari Samia Suluhu Hassan, ambapo amempongeza diwani mteule kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kwa kura nyingi na wananchi wa kata ya vibaoni na amemuahidi ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwake na Baraza zima la madiwani wa Halmashauri ya mji  Handeni.


Na mwandishi wetu

Handeni Mji

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI UJENZI WA JENGO LA DHARURA (EMD) HOSPITALI YA WILAYA HANDENI February 16, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • Afisa elimu msingi: Kula shuleni ni lazima

    March 13, 2023
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yafana, Halmashauri ya Mji Handeni

    March 08, 2023
  • Walimu Halmashauri ya Mji Handeni, wapata mafunzo ya mfumo wa FFARS

    March 04, 2023
  • MILIONI 63.6 ZAMWAGWA KWA WAJASIRIAMALI HANDENI MJI. RAIS SAMIA ATAJWA.

    March 03, 2023
  • Angalia zaidi

Video

Mbunge wa jimbo la Handeni Mjini Mh.Reuben Kwagilwa aliamsha Bungeni
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Kumuona Mkurugenzi
  • Kupata kibali cha Matangazo
  • Muundo wa Tasisi
  • Kumuona Mwenyekiti wa Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Sekretariti ya Ajira
  • Ofisi ya Rais - Ikulu
  • FFARS-LIVE
  • PLANREP- BAJETI 2020/21
  • TAMISEMI
  • Utumishi

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani

Wasiliana na sisi

    Barabara ya Korogwe - Handeni

    Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI

    Simu ya Mezani: 027-2641807

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: td@handenitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.