IDARA YA FEDHA NA BIASHARA.
Idara ya Fedha na Biashara ina majukumu yafuatayo yaliyogawanyika kama ifuatavyo;
MAJUKUMU YA IDARA YA FEDHA
• Kushauri Halmashauri kwenye masuala yote ya Fedha
• Kuandaa Makisio ya mwaka ya mapato na matumizi kwa kushirikiana na idara zingine zilizopo Halmasauri
• Kuandaa Ripoti za kawaida kwa Halmashauri kuhusiana na maendeleo ya matumizi halisi na Mapato kwa kulinganisha na Makisio ya Mwaka husika,na kutoa mapendekezo ya namna ya kutumia kulingana na kipato kilichopo
• Kuandaa Hesabu za Mwisho wa Mwaka na kutoa taarifa
• Kuhakikisha ufanisi wa udhibiti wa ndani katika kufuata sheria na taratibu za fedha,ikiwemo kuandika na kuzipitia mara kwa mara taratibu za fedha,kuziwasilisha kwenye kikao cha kamati ya fedha,uongozi na mipango kwa ajili ya kuidhinishwa na kugawanywa kwa wakuu wa idara
• Kufundisha Maswala yote yanayohusu matumizi mazuri ya Fedha kwa Halmashauri.
KITENGO CHA BIASHARA.
1. Shughuli za Seksheni ya Biashara viwanda na masoko
2. Sekisheni hii ni miongoni mwa nyenzo muhimu ndani ya Halmashauri ya Handeni katika kutekeleza Dira na Dhima ya Halimashauri.
3. Majukumu makubwa ya Seksheni.
4. Kusimamia na kuratibu shughuli za Biashara ndani ya Halmashauri,kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya wilaya,kutoa taarifa za masoko kwa Wafanyabiashara na wazalishaji wa ndani na nje
5. Kufanya ukaguzi wa maeneo ya Biashara,
6. Kutoa leseni za Biashara na vileo,
7. Kuandaa takwimu za Biashara na Masoko,
8. Kuratibu na kusimamia shughuli za uwekezaji.
Huduma mbalimbali zinazotolewa na zinazopatikana idara ya Fedha na Biashara ni;
• Elimu ya mlipa kodi ; Idara inatoa elimu hii kwa njia ya mbalimbali ikiwemo vipeperushi, matangazo kwenye redio,Televisheni na magazeti.
• Huduma za malipo mbalimbali ya watumishi na watoa huduma katika Halmashauri.
• Leseni za biashara mbalimbali katika Halmashauri zinapatikana katika kitengo cha Biashara.
• Vitendea kazi vya kukusanyia mapato kama stakabadhi za kupokelea mapato, mashine za kielektroniki(POS Machine)
• Ukusanyaji wa vyanzo vyote vya mapato ya halmashauri
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.